Tuesday, 22 April 2014

RAIS KIKWETE AKERWA NA WANASIASA WANAOMTUKANA NYERERE..SOMA ZAIDI HAPA...!!


 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
    
Rais Kikwete akerwa na kitendo cha wanasiasa kumtukana Mwalimu Nyerere....Asema ni utovu wa nidhamu kuwatukana waasisi wa Tanzania...


ASKOFU MKUU KKT IRINGA ASEMA:”UKAWA MARUFUKU KUKANYAGA IRINGA”


ASKOFU MKUU KKT IRINGA ASEMA:”UKAWA MARUFUKU KUKANYAGA IRINGA”
Na Francis Godwin, Iringa
ASKOFU mkuu wa Kanisa la Kilutheri (KKT) dayosisi ya Iringa Dkt. OwdenburgMdegela ameitumia ibada ya Jumapili ya Pasaka leo kulaani vikali wale wote wanaowatukana waasisi wa Taifa hili Sheikh Abeid Amani Karume na Mwalimu hayati Julius Kambarage Nyerere.
Askofu Dkt Mdegela amesema kuwa watu hao wanapaswa kuwaomba radhi watanzania huku akisisitiza wajumbe umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) kurejea bungeni ama kufungasha virago vyao na kurudi nyumbani kwao na sio kuzunguka kupandikiza chuki kwa wananchi.
Askofu Dr Mdegela, ambaye pia ni mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, aliyasema hayo leo wakati akitoa salam za pasaka kwa waumini wa Dayosisi hiyo kupita washarika wa kanisa kuu.
Dkt. Mdegela asema “Watanzania tunataka kuikataa lulu tuliyopewa na Mungu lulu ya amani na kuanza kutafuta kuvuruga amani na utulivu wetu ambayo ni lulu ya pekee inayogombewa na nchi nyingine na kuwa wanaotaka lulu hiyo ivurugike wasivumiliwe kamwe.
“Kinachofanywa bungeni kwa sasa ni mzaha wa hali ya juu na Watanzania wanapaswa kuwachunguza vema wawakilishi wao hao wakiwemo wabunge wa vyama vyote na wale wanaoeneza mbegu ya chuki wasichaguliwe tena….”
Asema wajumbe wa bunge la katiba hawana sifa ya kutengeneza katiba kwani wametanguliza mzaha na matusi yasiyo na tija na kuwa hawa wanaokwepa bunge na kutaka kuzunguka kwa wananchi wanapaswa kuzuiwa kufanya hivyo na vyombo vya usalama kwani wanataka kuipeleka nchi pabaya.
“Kama wamekula pesa za wananchi kwa muda wote huo kwa ajili ya kuunda katiba iweje leo watoke bungeni na kudai kuja kwa wananchi mikono mitupu??” amehoji.
“Wananchi tuwakatae wajumbe wanaotaka kuzunguka kupandikiza chuki kwa wananchi kwa kujiita wao wapo kwa ajili ya katiba ya wananchi hali wamekimbia bunge na kutaka kutuwakilisha nje ya bunge
“….tunawakataa wao na mawazo yao na pia kama wajumbe wa bunge hilo wameshindwa kazi tutaikataa rasmu ya katiba ambayo italenga kutugawa watanzania.
“Na niweke wazi mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Jaji Joseph Warioba mbali ya kazi hiyo bado tunawajibu wa kumrekebisha pale alipokosea kwani Wazanzibar wa Pemba wanataka serikali nne sio tatu mbona hajaeleza
” ….nasema serikali mbili ni jibu kama haiwezekani bado tuwe na serikali moja itakayotuunganisha”
Hata hivyo Dr Mdegela alisema kuwa msimamo wake na waumini wa kanisa hilo ni kuwa na serikali mbili na ikiwezekana kuwa na serikali moja pekee na si vinginevyo na iwapo wajumbe wa bunge la katiba wameshindwa kazi na kugeuza bunge hilo ni sehemu ya kuonyeshana ujuzi wa kutukanana ni vema wakirudi katika mwelekeo mzuri ama kurudi majumbani kwao ili viongozi wa dini mashekhe na maaskofu wakaifanya kazi hiyo ya kuunda katiba bila kutukanana .
“Nimejizuia sana kwa kipindi hiki cha bunge la katiba nisiseme chochote ila kutokana na mambo jinsi yanavyokwenda uvumilifu umenishinda nimelazimika kusema na ninachosema nimekiandika ili wale wapotoshaji washindwe kupotosha ninachosema….wayahudi walikataa kuongozwa na Samweli kwa sababu walisema watoto wa Samweli wanatabia mbaya …walikataa kuongozwa na Mungu kwa madai kuwa na wao wanataka mfalme wetu uli tukienda kupigana na watu ili tuwe kama mataifa mengine ila Mungu hakutaka wao kuwa kama mataifa mengine ila wao wanataka kuwa kama mataifa mengine ….Samweli akaenda mbele ya Mungu akilia ….ila Mungu akasema hawajakukataa wewe wamenikataa mimi …enyi watanzania tukikataa lulu tuliyopewa na Mungu ya kuwa nchi ya amani tutakuwa hakuwakatai viongozi wetu tutakuwa tunamkataa Mungu”
Aliwataka watanzania kuyatazama mataifa jirani kama Kenya ambao walijipenda wao na kushindwa kuwapenda majirani sasa Wasomari wameingia wanawasumbua ila tazameni pia Malawi ambao walimtaka rais wao awe Joys Banda ila alipoingia tu Ikulu alitangaza ndoa za jinsia moja pamoja na nchi ya Kongo ambayo imesaidiwa na Tanzania kurudi katika amani ikiwemo nchi ya Burundi ambayo Rais wake amekuwa akishinda katika maombi kwenye kanisa lake na kuacha kuongoza nchi.
“Tunapaswa kujiuliza amani hii iweje leo ichezewe na watu wachache wenye uchu wa madaraka na hata kususa bunge la katiba …hatujifunzi kutoka nchi za majirani zetu kama Uganda ,Rwanda kuna vyama 10 vya upinzani na kuna vikundi 10 vinavyotaka kumpindua Rais huku Uganda kuna mtu anaitwa Kony yeye siku zote kumshumbua Rais ….ninyi ni nani Tanzania bara na visiwani mkaa kwenye amani kiasi hiki na mnakataa umoja na kuanza kuwasikiliza wanaopandikiza mbegu ya kuvuruga amani ya kutaka serikali tatu ….watanzania tunataka kuikataa lulu tuliyopewa na Mungu lulu ya amani”
Dr Mdegela alisema kuwa hadi sasa mwenendo wa bunge la katiba unatia aibu kubwa kwa Taifa na hata nje ya taifa hili na kuwataka wajumbe hao kuwa wasikivu na kama walisema wanakwenda kuandaa katiba ya wananchi iweje kabla ya kuanza kwa bunge hilo walianza kwa kulilia posho kuongezwa hali wakijua walimu hawajalipwa malipo yao pamoja na wafanyakazi hawajaongezwa mishahara yao.
“Natamka wazi kuwa mimi Dr Mgedela sina imani hata kidogo na wajumbe wa bunge la katiba …..kama wanavyoonekana na walivyo wana hadhi ya kutoridhika watatuletea katiba mbovu kwa sasa na wao ni wabovu ..
“Natamka rasmi kuwa tume iliyoandaa rasmi ya katiba haukuandaa msaafu wala Biblia ili andaa kitu ambacho mbacho kinaweza kuhojika na kukataliwa ama kukubalika wao si Miungu ni wanadamu kama sisi madai kuwa wanavyeo vingi serikalini hata mfagiaji anavyo ….sasa naiomba serikali hao waliojitoa bungeni wanataka kuja kwa wananchi tunasema hatuwataki ….
“Hivi kama mtu ameshindwa kujenga hoja bungeni watakuja kutueleza nini nawaombeni usalama wa Taifa fanyini kazi ya kulinda amani yetu ….kama hawataki kurudi bungeni basi waende majumbani kwao”
Askofu Dr Mdegela alisema kanuni za bunge wametunga wao na iweje leo wanakimbia kanuni waliyoitunga hivyo kama wanaona kanuni ni mbaya basi watuombe Watanzania wenye akili tuwasaidie hata yeye anaweza kwani wajumbe hao ni walafi wasiopenda amani ya nchi hii.
Katika hatua nyingine askofu huyo alisema kwa sasa kinachoendelea na kuwa kila kanda itataka serikali yao iwapo hoja ya serikali tatu ikapitishwa.
  • Kan 1
  • Kan 2

MAKOSA WANAYOFANYA WANAUME WALIO KWENYE NDOA

1- Kuja na vimada mpk home na kumuacha ndani ya gari

2-Kuingia ndani na viatu vya matope wakati
kumeshadekiwa

3-Kuvurugua nguo au vitu wakati wa kutafuta kitu kabla ya kuuliza kilipo.

4-Kumtambulisha mtoto wako kwa kimada wako.

5-Kumleta rafiki yake kuja kula bila kutoa
taarifa.

6-Kumsifia rafiki au ndugu wa mke wa kike
kuwa anavutia bila hofu.

7-Kukosoa muonekano wa mke bila kujali
atajisikiaje.

8-Kutosema chochote mke akipendeza mpaka aulize.

9- Kujifutia taulo na kuliacha ovyo bila kulianika

10- Kutotandika bed mke asafiripo na kugeuza bed kama kiota cha ndege

11-Kutofua boxer na socks zake hadi wife
awepo na kama kasafiri zitasubiri arudi

WEMA AWAJIBU WANAOMPONDA BAADA YA KUSHINDA TUZO YA IJUMAA SEXIEST GIRL


Tangu akabidhiwe tuzo yake ya Ijumaa sexiest girl, Mrembo Wema Isaac Sepetu 'Beautiful Onyinye' tayari inaonekana ameshakutana na negative comments baada ya kushinda hiyo tuzo.

1
Wema Sepetu ameibuka mshindi katika shindano la Ijumaa Sexiest Girls akiwabwaga Lulu, Nelly, Wolper, Jokate.
Wema ametumia ukurasa wake wa instagram kutoa yaliyo moyoni mwake na ameandika,
“If u got it flaunt it….. Ndo nshashinda…. kama hujapenda kasage chupa kunywa…. maana naona sasa its too much khaaaaaaaa.!
Ebu mnitue mie mtoto wa watu… And again much love to y’all dat support me… nawapenda sana…. nimemaliza…. Award yangu ndo hiiiiiiiiooooooooo…… next year tusubiri mwingine.
Nalala zangu…. tukutane kesho…. najua wengi mnanipenda ni wachache wenye vijiba vyao vya roho…. Wema atabaki kuwa Wema tu… Bhaaaaas.”

BAADA YA KIMYA KIREFU HATIMAYE MASOGANGE ATOBOA SIRI KUMHUSU JAMAA ALIYEMPA MADAWA ALIYOKAMATWA NAYO SOUTH


‘VIDEO queen’ wa Kibongo, Agness Gerald, ‘Masogange’, amefunguka  kuwa aliyempa mzigo wa unga  na akakamatwa nao nchini Afrika Kusini, alikuwa amevalia kininja, hali iliyomfanya ashindwe kumtambua.

 Taarifa za uhakika kutoka vyanzo vyetu makini katika kikosi kazi cha kuzuia na kudhibiti madawa ya kulevya nchini (Task Force), zinasema kuwa  mwanadada  huyo alipofika katika nchi hiyo, alipigiwa simu na mtu ambaye hamjui aliyemwambia kuwa atapewa mzigo, hivyo ajiandae kuupokea.

“Alidai kuwa kuna mtu aliyevalia kininja alifika eneo alilokuwepo uwanjani pale ambaye hakumsemesha badala yake alimpatia mzigo wa unga ambao ulikuwa kilo 150 ambao hapa kwetu ni madawa ya kulevya na kuondoka kusikojulika,” kilisema chanzo.
 Kwa upande wake, Kamanda wa Kudhibiti na Kupambana  na Madawa ya Kulevya nchini,  Godfrey Nzowa alipohojiwa na gazeti hili alithibitisha kuwa Masogange aliwaeleza polisi wa Afrika Kusini kuwa aliyempa unga ule ni mtu aliyekuwa amevalia kininja.

SABABU ZA UGOMVI BAINA YA MAPACHA WA P-SQUARE ZAFAHAMIKA, SOMA HAPA

Taarifa juu ya ugomvi ulioibuka wiki iliyopita baina ya ndugu mapacha wa kundi la P-Square Peter na Paul na kaka zao zimewashtua mashabiki wao walioko pande mbalimbali za dunia. Chanzo kimoja cha karibu na ndugu hao kimeelezea sababu na kile kilichotokea.

Inadaiwa kuwa ugomvi wa wanandugu wa familia ya Okoye ulianzia kwa wasaidizi wao binafsi, ‘Personal Assistants’ (PA’s).
 Ripoti kutoka katika vyanzo mbalimbali vya Nigeria zinasema kuwa ‘PA’ wa kaka yao mkubwa Jude aitwaye Wande alimpatia ‘PA’ wa Peter aitwaye Shege, pesa ili akamsajilie gari lake, lakini inasemekana ‘PA’ wa Peter badala ya kutumia pesa hizo kwa kazi aliyoelekezwa alizitumia kwa kitu tofauti. 
 Baada ya hapo inadaiwa kuwa ‘PA’ wa Jude alikasirika baada ya kugundua kuwa pesa alizompa ‘PA’ wa Peter hazikufanyiwa kazi aliyoelekeza. Alipoenda nyumbani kwa Okoye’s ‘Squareville’ ili kukabiliana na ‘PA’ wa Peter ndipo ugomvi ulizuka baina ya wasaidizi hao wawili wa ndugu.
 Chanzo kinaendelea kusema baada ya ugomvi kuanza Peter aliingilia na kutaka kumpiga msaidizi wa Jude hadi Paul alipoingilia kwa lengo la kuwaachanisha, lakini badala yake Peter alijikuta akimpiga ngumi pacha wake Paul na kuanguka chini japo inadaiwa kuwa Paul hakumrudishia ngumi kaka yake, na badala yake kaka yao mwingine aitwaye Tony naye aliingilia na kuanza kupigana na Peter. Wakati haya yote yanatokea mke wa Paul Anita alikuwa akishuhudia.
 Chanzo kiliongeza kuwa Peter anataka awe mhusika mkuu wa maswala ya fedha za kundi au apate mgao mkubwa zaidi, huku upande wa pili inadaiwa Paul anataka kaka yao mkubwa ambaye pia ni meneja wao Jude aendelee kuwa msimamizi mkuu wa maswala ya fedha zao kama ilivyokuwa miaka yote iliyopita, lakini mpaka ilifikia hatua ya kutaka wagawane mali kila mtu awe na chake.
 Baada ya habari za ugomvi baina ya wana ndugu hawa kuenea, hii ni post ya Paul aliyoiandika juzi kupitia ukurasa wake wa Facebook. 
 “After the storm comes the calm. Hoping for better days ahead as one family. God’s intervention.”
BONGO 5

SITTA AIFUATA UKAWA ZANZIBAR KUNUSURU BUNGE

Wakati viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wakiweka kambi Zanzibar, Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta jana naye alitumia siku nzima visiwani humo akikutana na baadhi ya viongozi wa Serikali, katika kile kinachotafsiriwa kuwa kulinusuru Bunge hilo.

Habari zilizolifikia gazeti hili kutoka Zanzibar zinasema Sitta alikutana na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad, Rais Mstaafu, Aman Karume na mwanasiasa wa siku nyingi wa CCM, Mzee Hassan Nassor Moyo.

Zanzibar kwa sasa ndiyo moyo wa upatikanaji wa Katiba Mpya kutokana na wajumbe wake katika Bunge kutegemewa ama kuipitisha au kuikwamisha kwa kuwa kila upande kati ya mbili zinazovutana, hauna uhakika wa kupata theluthi mbili za kura.

Baada ya kuondoka bungeni na kutangaza kususia vikao vya Bunge hilo Aprili 16, mwaka huu, siku mbili baadaye viongozi wa Ukawa waliingia Zanzibar wakitaka kufanya mikutano ya hadhara kuwaeleza wananchi sababu za kufanya hivyo, lakini wakazuiwa na polisi na hadi jana walikuwa wanasubiri kibali.

Safari ya Sitta

Katibu wa Bunge Maalumu, Yahya Khamis Hamad pamoja na kuthibitisha ziara ya Sitta Zanzibar kuwa alikuwa akutane na Dk Shein, alisema hafahamu lolote kuhusu mkutano wake na Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF.

“Sifahamu malengo ya safari wala walichokwenda kuzungumza, ila ni kweli kwamba alifika Zanzibar leo (jana) na alitarajiwa kuondoka jioni kurejea Dodoma,” alisema Hamad na kuongeza:

“Hilo la kuonana na Maalim Seif silifahamu ila ninachojua aliniambia nimfanyie miadi ya kuonana na Dk Shein na nikaifanya kama alivyoelekeza.”

Mapema habari zilizolifikia gazeti hili kutoka Zanzibar zilisema, Sitta baada ya kukutana na Karume, Shein na Mzee Moyo alitarajiwa kukutana na Maalim Seif saa 9:00 alasiri.

Katibu wa Maalim Seif, Issa Kheri Hussein alithibitisha kwamba Sitta alikutana na kiongozi huyo nyumbani kwake, Mbweni saa 9:30 alasiri jana, lakini alidai kutokuwa na taarifa za mazungumzo hayo.

“Hilo naweza kulithibitisha kwamba mkutano huo umefanyika lakini mazungumzo yenyewe yalikuwa ya faragha na mimi baada ya Sitta kufika niliondoka, hivyo sikuweza kufahamu kilichozungumzwa kwa undani, pengine mpaka nizungumze na Maalim mwenyewe,” alisema Hussein.

Ziara ya Sitta kwenda Zanzibar imekuja wakati ambao kumekuwa na wasiwasi mkubwa wa kukwama kwa vikao vya Bunge hilo kutokana na msimamo wa Ukawa.